×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

115 WADAKWA KWA MATUKIO YA KIHALIFU MWANZA

Na Mwandishi wetu.

Jumla ya watuhumiwa 115 wa makosa mbalimbali ya kihalifu ikiwemo makosa ya wizi wa Samaki, kuishi nchini bila kibali, kupatikana na nyavu haramu sanjari na matumizi ya bangi wamekatwa na Jeshi la polisi kufuatia msako uliofanyika kwa kipindi cha siku tano, katika visiwa mbalimbali vilivyopo ndani ya Ziwa Victoria.

Taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Naibu Kamishina wa Polisi DCP Wilbroad Mutafungwa amesema, msako huo umefanyika kuanzia Januari 15 hadi 20 mwaka huu katika visiwa vya Yozu, Nyamango, Soswa na maeneo ya Kanyala na Mbugani katika kata ya Bulyaheke Halmashauri ya Buchosa mkoani Mwanza.

#NTTUpdates