Na Mwandishi wetu.
Kiungo wa timu ya Taifa ya Hispania na klabu ya Barcelona Aitana Bonmati Conca (26) ametwaa tena tuzo ya Ballon d’Or 2024 akiwashinda Caroline Graham Hansen na Salma Paralluelo wote wakiwa wachezaji wa Barcelona ya wanawake.
Aitana Bonmati anaibeba tuzo yake ya pili mfululizo ya Ballon d’Or baada ya kuwa na msimu Bora na kupeleka mafanikio makubwa kwenye klabu yake ya Barcelona na timu ya Taifa ya Hispania.
#NTTupdates