Na Mwandishi wetu.
Klabu ya Al Ahli SC inayoshiriki ligi kuu ya Saudi Arabia (Saudi Pro League), imefanikiwa kunasa saini ya winga wa kushoto Wenderson Rodriguez do Nescimento Galeno (27) raia wa Brazil akitokea FC Porto ya Ureno.
Nyota huyo ambaye alikuwa akihusishwa na Mabingwa watetezi wa ligi kuu Uingereza (EPL) Manchester City lakini dili hilo limeota mbawa baada ya kushindwa kukamilisha dili hilo.
Galeno akiwa na Porto FC msimu huu amecheza michezo 31 akifunga magoli 12 na kutoa assist 3 kwenye michuano yote ambayo klabu hiyo imeshiriki.
Al Ahli SC imeendelea kujiimarisha kwenye eneo lao la ushambuliaji ambapo Galeno atajiunga na Ivan Toney, Mahrez na Roberto Firmino.
#NTTupdates