×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

ALEX MORGAN KUSTAAFU KANDANDA

Na Mwandishi wetu.

Nahodha wa timu ya Taifa ya wanawake ya Marekani na klabu ya San Diego Wave, Alexandra Morgan Carrraso (35) maarufu kama ” Farasi mtoto”

jina alilopewa na wachezaji wenzake wa timu ya Taifa kutokana na mikimbio yake akiwa uwanjani, ametangaza rasmi kustaafu kucheza soka la kulipwa.

Nyota huyo alirekodi video fupi kwenye mtandao wa kijamii ambapo aliweka wazi kuwa anastaafu kucheza soka, pia akitangaza kuwa ana ujauzito wa mtoto wa pili na mwenza wake Servando Carrasco.

Alex Morgan ambaye yupo kwenye rekodi ya wachezaji 5 walioifungia magoli mengi timu ya Taifa ya wanawake ya Marekani ambayo rekodi hiyo inaongozwa na 1.

Mary Abigail Wambach maarufu kama Abby Wambach ambaye aliichezea Marekani michezo 224 na alifunga magoli 184 kuanzia mwaka 2001-2015.2.

Mariel Margaret maarufu kama kama Mia Hamm mshambuliaji ambaye alitumikia Taifa hilo kwenye michezo 276, akifunga magoli 158 kuanzia mwaka 1987-2004.3.

Carli Anne Hollins ambaye alikuwa akicheza nafasi ya kiungo mshambuliaji au mshambuliaji wakati mwingine aliicheza Marekani michezo 316 na kufunga magoli 134 kuanzia mwaka 2005-2021.4.

Kristine Marie Lilly Heavey mshambuliaji huyo aliitumikia Marekani kwenye michezo 154 akifunga magoli 130 kuanzia mwaka 1987-2010.5. Alexandra Morgan Carrraso.

ambaye ameitumikia Marekani kwenye michezo 224, akifunga magoli 123 na kutoa assist 53 kuanzia mwaka 2010-2024.

Mshambuliaji huyo amefanikia kutwaa mataji mbalimbali ya soka barani Ulaya na America kwa ujumla ambapo akiwa na timu yake ya Taifa ya Marekani aliwahi kubeba kombe la Dunia kwa vijana U-20 mwaka 2008 na baadae alibeba kombe hilo timu ya wakubwa mwaka 2015 na 2019, Medali za Olympic mwaka 2012 ya dhahabu na 2020 ya fedha na makombe kadha ya kama CONCACAF mara tatu mfululizo 2014, 2018 na 2022 na michuano mengineyo kwenye bara la Amerika.

Kwa upande wa vilabu Alex Morgan ametwaa makombe kadhaa yakiwemo ligi ya Mabingwa Ulaya kwa wanawake akiwa na Lyon msimu wa 2016- 2017, Ngao ya jamii 2023 na Challenges cup 2024 akiwa na San Diego Wave Marekani.

Alex Morgan ametangaza mchezo wake wa mwisho utakuwa siku ya jumapili Septemba 8, 2024 ambapo klabu ya San Diego Wave itacheza na North Carolina Courage.

# San Diego Wave

#NTTupdates