Na Mwandishi wetu.
Mwamuzi wa Tanzania Ahmed Arajiga kutoka Manyara, ameteuliwa na shirikisho la soka Afrika CAF kuwa miongoni mwa Waamuzi watakaochezesha mchezo wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL) kati ya Pyramids FC ya Misri dhidi ya FC FAR ya Morocco utakaochezwa kwenye uwanja wa 30 June, jijini Cairo nchini Misri Aprili 1, 2025.
Arajiga ambaye amekuwa na uzoefu mkubwa wa kuchezesha mechi kubwa hasa za Derby ya Kariakoo na Mzizima Derby lakini pia mechi za michuano ya kufuzu CHAN na AFCON.
#NTTupdates