Na Mwandishi wetu.
Athari za mabadiliko ya tabianchi zinazotokana na shughuli mbalimbali za binadamu zatajwa kuwa chanzo cha moja Kwa moja Cha watu wengi hapa nchi kuugua magonjwa ya ngozi.
Kauli hiyo imebainishwa na Daktari bingwa wa magonjwa ya ngozi kutoka hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando Daktari Nelly Mwageni, amesema kuwa Changamoto za ngozi zipo nyingi lakini nyingine zinachangiwa na mabadiliko ya hali ya hewa, kutokana na shughuli zinazofanyika katika viwanda,uchafuzi wa mazingira kwani vinaleta vumbi pamoja na hewa chafu ambavyo vinaleta madhara ya moja kwa moja kwenye ngozi sababu ngozi ndio kiungo ambacho kipo nje ya mwili wa mwanadamu ambacho ndicho sehemu kubwa ya ulinzi wa mwili.
Amebainisha kuwa zaidi ya watu mia mbili (200) wamejitokeza katika zoezi la uchunguzi, elimu na matibabu ya Afya ya ngozi kutoka kwa madaktari bingwa wa ngozi wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando.
“Hospitali ya Bugando kila siku inapokea zaidi ya wagonjwa wa ngozi hamsini (50), ndio maana tumewiwa kutoa huduma ya matibabu ya ngozi, elimu na ushauri wa afya ya ngozi”, Amesema Daktari Nelly.
Sambamba na hayo Daktari Nelly ametoa wito kwa wananchi wote kutibu magonjwa ya ngozi kwa uzito na uharaka, kwa matibabu sahihi.
Baadhi ya magonjwa hayo ya ngozi ni pamoja na Vipele, pumu ya ngozi, muwasho wa ngozi, Fangasi, Magonjwa ya kucha na nywele pamoja na Magonjwa ya maambukizi kwenye ngozi.
#NTTupdates