Na Mwandishi wetu.
Klabu ya Aston Villa imemtambulisha mlinzi wa kati Axel Witson Athur Disasi Niforas Disasi (26) raia wa Ufaransa ambaye amejiunga na klabu hiyo kwa mkopo akitokea klabu ya Chelsea.
Aston Villa inaendelea kujiimarisha kwenye eneo lao la ulinzi kwa ujio wa Disasi ili waweze kufanya vizuri msimu huu kwenye ligi kuu ya Uingereza (EPL).
Msimu huu pekee Disasi aliichezea Chelsea michezo 17 akifunga magoli 2 na kutoa assist 2 kwenye michuano ambayo klabu hiyo ilishiriki.
#NTTupdates