Na Mwandishi wetu.
Baada ya kuvuna mabilioni ya fedha Ulaya na Asia Mfungaji Bora wa muda wote wa timu ya Taifa ya Brazil Neymar Jr (32) amerejea rasmi kwenye klabu yake ya utotoni ya Santos FC iloyopo kwao Brazil ambapo amesaini mkataba wa miezi 6.
Neymar Jr aliondoka kwenye klabu hiyo akiwa kijana mdogo wa miaka 21 na kutimkia Ulaya kwenye klabu ya Barcelona na kupata mafanikio makubwa kwenye soka ikiwemo kubeba kombe la ligi ya Mabingwa Ulaya (UEFA).
Pia aliwahi kupita PSG ya Ufaransa, nyota huyo ameamua kujiunga na Santos baada ya kuvunja mkataba na klabu ya Al Hilal ya Saudi Arabia kutokana na majeraha yake.
#NTTupdates