Na Mwandishi wetu.
Mkuu wa Wilaya ya Babati Emmanuela Mtatifikolo Kaganda, leo Disemba 09, 2024 amewaongoza wananchi na watumishi wa Wilaya ya Babati kuadhimisha miaka 63 ya Uhuru wa Tanzania kwa upandaji wa miti.
Kaganda amewataka wananchi wa Babati na Tanzania kwa ujumla kuitumia siku hii ya Disemba 09 kuwaombea viongozi wote waliyoshiriki na kuhakikisha Tanzania inapata Uhuru wake wakiongozwa na Hayati Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambaraga Nyerere ambaye alikuwa mstari wa mbele katika kufanikisha Uhuru wa Tanzania unapatikana.
Katika hatua nyingine ya kuadhimisha miaka 63 ya Uhuru wa Tanzania wananchi wa Babati wameshiriki kwenye shughuli mbalimbali za kijamii ikiwemo kukimbia mbio fupi za pamoja, kupanda miti ya matunda na kivuli katika hospitali ya Halmashauri ya Mji wa Babati pamoja na kutoa zawadi kwa wazazi na wajawazito.
#NTTupdates