Na Mwandishi wetu.
Dakika 90 zimemalizika kwenye uwanja wa KMC Complex Mwenge jijini Dar es Salaam na kushuhudia Wananchi Young Africans SC wakipata ushindi wa magoli 8-1 dhidi ya Chama la Wana Stand United na kutinga hatua ya nusu fainali ya kombe la FA la CRDB.
Mchezo huo ulishuhudia Kiungo mshambuliaji Aziz Ki akiweka kambani magoli manne dakika ya 16′, 51′, 60′ na 64′ pia nyota Cletus Chota Chama akiweka kambani magoli 2 dakika ya 32′ na 41′ huku magoli mengine yakifungwa na Nickson Kibabage dakika ya 20′ na mshambuliaji Kennedy Musonda dakika ya 87′ huku goli pekee la kufutia machozi la Stendi United likiwekwa kambani na Msenda Senda dakika ya 49′.
Baada ya ushindi huo kwa wananchi Young Africans SC watakutana na JKT Tanzania kwenye mchezo wa nusu fainali wa kombe hilo.
#NTTupdates