Na Mwandishi wetu.
Aliyekuwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Upelelezi wa Fedha huko Guinea ya Ikweta (ANIF), Baltasar Ebang Egonga Avomo (47), amehukumiwa jela miaka 18 baada ya kukutwa na hatia ya Rushwa na ubadhirifu wa fedha za Umma.
Hukumu hiyo imetolewa hapo jana Jumatano Julai 2, 2025, ambapo Mahakama kuu jijini Malabo ilibaini Baltasar aliiba zaidi ya Dola za Marekani Milioni 1.5 kutoka kwenye mfuko wa Umma na kuzificha kwenye Akaunti za Benki za nje ya nchi hiyo.
Upotevu huo wa fedha za Umma ulithibitishwa kupitia Ukaguzi wa miamala ya Benki, Akaunti za ofisi za kigeni pamoja na mikataba hewa ambayo Baltasar alitia Saini.
Pia Baltasar amekutwa na hatia ya kutumia ofisi ya Umma kwa manufaa yake binafsi, ikiwemo kufanya vitendo visivyofaa ndani ya ofisi na kutumia madaraka yake vibaya kwa kuwalaghai kingono baadhi ya wanawake walikuwa wakitaka Ajira au kupandishwa vyeo kwenye idara hiyo.
Mpwa huyo wa Rais wa Equatorial Guinea, Toedoro Obiang Nguema alijipatia umaarufu baada ya kusambaa kwa video zake za Faragha akiwa na Wanawake zaidi ya 400 kwenye sehemu zaidi ya moja, huku wengine wakiwa watu maaarufu nchini humo na kushangazwa watu wengi kutokana na wadhifa wake.
#NTTupdates