×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

BARCELONA BINGWA SUPER CUP HISPANIA

Na Mwandishi wetu.

Barcelona imeendeleza ubabe wake kwenye michezo ya El Clasico kwa mara ya pili mfululizo baada ya kupata ushindi wa magoli 5-2 kwenye mchezo wa fainali ya Super Cup dhidi ya mahasimu wao Real Madrid.

Magoli ya mchezo huo kwa upande wa Real Madrid yamefungwa na Kylian Mbappe dakika ya 5 na Rodrigo dakika ya 60 huku magoli ya Barcelona yakifungwa na Yamal dakika ya 22, Lewandowski dakika ya 36, Raphinha aliyefunga magoli mawili dakika ya 39 na 48 huku goli la Tano likifungwa na na Balde dakika ya 45+10.

Mchezo huo pia ulishuhudia nyota wa Real Madrid Kylian Mbappe akiweka rekodi ya kufunga goli lake la kwanza kwenye mchezo wa El Clasico toka ajiunge na Real Madrid mwanzoni mwa msimu huu akitokea PSG.

Barcelona chini ya Hans Flicks imeshinda michezo miwili mfululizo ya El Clasico ambapo kwenye La Liga waliwafunga Real Madrid magoli 4-0 na kwenye fainali wakishinda tena 5-2 na kubeba taji lao la kwanza msimu huu na kuendeleza ubabe kwa Carlo Ancelott.

#NTTupdates