Na Mwandishi wetu.
SERIKALI imetenga Shilingi bilioni 123.92 kwa ajili ya utoaji wa mikopo kwa wanawake, vijana na watu wenye ulemavu kupitia halmashauri mbalimbali lengo likiwa ni kuwawezesha wananchi kiuchumi.
Hayo yameelezwa leo Aprili 16,2025 bungeni jijini Dodoma na Waziri wa nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mohammed Mchengerwa wakati akiwasilisha bajeti ya Ofisi hiyo katika mwaka wa fedha 2025/2026.
Mchengerwa amesema Shilingi bilioni 18.35 zitatolewa kupitia mfumo wa kibenki katika halmashauri 10 za mfano, huku Shilingi bilioni 105.57 zikitolewa kupitia mfumo wa serikali ulioboreshwa.
#NTTupdates