Na Mwandishi wetu.
Kamanda wa Polisi Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP) Virginia Sodoka, amewata waendesha bodaboda kuhakikisha wanaheshimu Sheria za usalama barabarani hili kupunguza ajali za barabarni.
Ametoa wito huo wakati akitoa elimu kwa maofisa usafirishaji kutoka Kata za Mkolani, Nyegezi na Luchelele huku akisisitiza umuhimu wa matumizi sahihi ya alama za barabara kwa lengo la kulinda usalama wa watumiaji wengine wa barabara.
Aidha, amewataka waendesha pikipiki kushirikiana na Jeshi la Polisi kwa kutoa taarifa za uhalifu, hasa wahalifu wanaotumia pikipiki kufanya vitendo viovu, kwani vitendo hivyo vinaharibu taswira ya sekta hiyo.
Pia amewakumbusha kuhakikisha wanakuwa na leseni halali na bima za vyombo vyao ili kuepusha usumbufu na adhabu kutoka kwa askari wa usalama barabarani na mamlaka nyingine za Serikali zinazosimamia sheria.
#NTTupdates