Na Mwandishi wetu.
Shirikisho la soka barani Afrika CAF limezindua kombe jipya litakalokuwa linatumika kwenye ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL) ambapo mshindi wa fainali atabeba taji hilo kwa mara ya kwanza.
Kombe hilo limezinduliwa leo Mei 22, 2024, nchini Afrika Kusini ambapo ndipo mchezo wa Mkondo wa kwanza wa Fainali ya ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Mamelodi Sundowns dhidi ya Pyramid ya Misri utapigwa Jumamosi Mei 24, 2025.
#NTTupdates