×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

DC ARUMERU AFANYA KIKAO NA KIKUNDI KINACHOENDA KUPATA MAFUNZO YA UFUGAJI KUKU

Na Mwandishi wetu.

MKUU wa Wilaya ya Arumeru Emmanuela Mtatifikolo Kaganda Agosti 23, 2024 amefanya kikao na kikundi kitakachopatiwa mafunzo ya ufugaji wa kuku kama fursa ya maendeleo katika Wilaya hiyo.

Kikao hicho ni matokeo ya kongamano lililofanyika Agosti 12, 2024 ambapo makundi ya wanawake walipatiwa elimu za fursa mbalimbali ikiwemo ufugaji wa kuku wa kisasa ambapo kampuni ya silver land iliahidi kutoa ufadhili wa mafunzo kwa wanawake 10 ikiwemo maafisa mifugo na wawakilishi wawili upande wa wanaume.

Katika kikao hicho baadhi ya wajumbe waliohudhuria wamesema baada ya kupata mafunzo hayo, itakuwa ni chachu kwenye miradi yao ya ufugaji wa kuku huku wakiahidi kuendeleza kuambukiza mafunzo watakayopewa kwa wafugaji wengine ili kuendeleza kukuza uchumi wa ufugaji wa kuku.

Kwa upande wake, Meneja wa Mauzo wa Ukanda wa Kaskazini wa Silver lands Bw. Meshack Msalege ameeleza baada ya mafunzo hayo kwa upande wa Arumeru itakuwa ni upendeleo wa pekee na kutakuwa na mabadiliko chanya kwenye eneo la ufugaji kwani wafugaji wengi wamekuwa wakifuga kimazoea kwahiyo kupitia mafunzo hayo yatawasaidia sa wafugaji wa hao kufanya ufugaji wa tija.

Aidha, Kaganda amesema kuelekea mashindano ya Afcon 2027 Mkoa wa Arusha utapata wageni wengi hivyo kupitia ufugaji huo wa kuku wafugaji watanufaika kwani kuku ni moja ya kitoweo kinachopendwa na watu wengi.

#NTTupdates