×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

DC KISWAGA AWATAKA MAAFISA RASILIMALI WATU KUTOA MBINU BORA KWA WATUMISHI

Na Mwandishi wetu.

Mkuu wa Wilaya ya Monduli Festo Kiswaga, amemuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Arusha Paul Christian Makonda leo Novemba 4, 2024 kwenye mkutano wa tisa wa Mtandao wa Mameneja na Wasimamizi wa Rasilimali Watu katika Sekta ya Umma Barani Afrika unaofanyika mkoani Arusha kwenye ukumbi wa Kimataifa wa mikutano Arusha ( AICC).

DC Kiswaga amesema kuwa Maafisa rasilimali watu wanajukumu kubwa la kuhakikisha watumishi wa Sekta ya Umma kusimamia ipasavyo rasilimali zote muhimu, ndani ya Bara la Afrika kwa kuandaa mazingira bora na wezeshi kwa wafanyakazi ikiwa ni pamoja na kukuza uwezo wa watumishi hao kwa kuvumbua na kuleta mabadiliko chanya ya utendaji wa kazi.

Aidha DC Kiswaga, amewataka viongozi wote wanaohusiku na usimamizi wa Rasilimali Watu kuwa na mbinu za kisasa zaidi zinazojumuisha maarifa, uadilifu na ufanisi katika kujenga watumishi wenye uwezo wa kustahimili changamoto mbalimbali zinazokwenda sambamba na mabadiliko ya teknolojia na mahitaji ya kiuchumi kwenye nchi zote za Afrika.

#NTTupdates