×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

DC KISWAGA AZINDUA KICHOMEA TAKA HOSPITALI YA WILAYA MONDULI

Na Mwandishi wetu,Arusha.

MKUU wa Wilaya ya Monduli Festo Kiswaga, Septemba 18, 2024 amezindua Kichomea taka chenye thamani ya million 43 katika hospitali ya Wilaya ya Monduli ikiwa ni miongoni mwa msaada kutoka shirika lisilo la Kiserikali la TANDIA.

Akizungumzia matumizi ya Kichomea taka hicho Eng. Kashimu S. Laizer ( Biomedical Engineer) amesema kifaa hicho kina faida kubwa ikiwa ni pamoja na kutunza mazingira lakini pia kulinda afya za watu walio karibu na mazingira hayo pia kuokoa muda kwa mchoma taka.

Sambamba na hilo DC Kiswaga amesisitiza kuwa, kifaa hicho kitasaidia kuondoa usumbufu mkubwa uliokuwepo wakati wa kuchoma taka ngumu zisizo ungua kwa haraka.

DC Kiswaga amehitimisha kwa kutoa shukrani zake za dhati kwa Shirika hilo lisilo la Kiserikali TANDIA kwa ujenzi wa Kichomea taka hicho katika hospitali ya Wilaya ya Monduli huku akisisitiza pia utunzaji mzuri wa Kichomea taka hicho ilikiendelee kudumu zaidi.

#NTTupdates