Na Mwandishi wetu.
Mkuu wa Wilaya ya Arusha Joseph Mkude leo Julai 30, 2025 ameambatana na kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa huo, pamoja na watendaji wa Wilaya kwaajili ya ukakuguzi wa ujenzi wa miradi mbalimbali ikiwemo ujenzi wa stendi mpya ya kisasa ya mabasi katika eneo la Bondeni City, ujenzi wa soko la Kilombero pamoja na ujenzi wa barabara ya Esso-Long Dong.
Katika ziara hiyo, Mkude amesema kuwa kamati hiyo imeridhishwa na kasi inayotumika katika utekelezaji wa miradi hiyo kwani miradi hiyo inatarajiwa kukamilika mwaka huu.
#NTTupdates.