Na Mwandishi wetu.
Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya ( DCEA) Kanda ya Kaskazini kwa kushirikiana na Sekretarieti ya maadili ya viongozi wa Umma Kanda ya Kaskazini imetoa msaada wa vifaa mbalimbali katikati nyumba za watu waliopata nafuu baada ya kutumia dawa za Kulevya zilizopo Olmotonyi na Moshono Jijini Arusha.
Lengo la msaada huo kwa waraibu hao ni kuwaonyesha kuwathamini na kuwatia moyo waraibu hao wanaoendelea kupata nafuu katika nyumba hizo pamoja na kuwaonyesha kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Rais.
Dkt. Samia Suluhu Hassan ipo pamoja nao katika mchakato wa kupona na uraibu wa dawa za Kulevya.
Aidha, Viongozi wa Ofisi za DCEA na Maadili Kanda ya Kaskazini wametoa wito kwa wananchi wa mkoa wa Arusha kuendelea kutunza maadili mema katika jamii kwani maadili mabaya ni chanzo cha maovu katika jamii.
#NTTupdates.