×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

DEDE AFUTURISHA WAANDISHI WA HABARI MWANZA .

Mwenyekiti wa chama cha madereva wa malori na mabasi ya Masafa Marefu Tanzania (TLDTA) Hassan Dede amewahimiza waandishi wa habari kufanya kazi kwa uzalendo kwa ajili ya nchi yao.

Dede ameyasema hayo wakati wa iftar mahususi aliyoandaa kwa ajili ya waandishi wa habari Jijini Mwanza

Amesema waandishi wa habari wana mchango mkubwa katika maendeleo ya katika nchi hivyo ameona ni vyema kujumuika nao pamoja kama ishara ya umoja mshikamano na upendo katika mwezi mtukufu wa Ramadhan na kwaresma.

Akizungumza kwa niaba ya Waandishi wa habari mkoani mwanza George Binagi amemshukuru Dede kwa kuthamini mchango wao kwani futari hiyo imeimarisha umoja na mshikamano kwa wanahabari na wadau mbalimbali jijini Mwanza.

NTTupdates .