Na Mwandishi wetu.
Kocha wa Timu ya Taifa ya Ufaransa Didier Claude Deschamps (56) raia wa Ufaransa ametangaza rasmi kuwa ataacha kuinoa timu ya Taifa ya Ufaransa baada ya kombe la Dunia la mwaka 2026 ambapo litafanyika katika mataifa matatu ya Marekani, Canada na Mexico na litakuwa la mwisho kuiongoza Ufaransa kusaka taji hilo.
Deschamps ameiwezesha timu ya Taifa ya Ufaransa kushinda kombe la Dunia mwaka 2018 nchini Urusi na kucheza fainali ya mwaka 2022 nchini Qatar licha ya kushindwa kutetea taji hilo mbele ya Argentina.
Ufaransa chini ya Deschamps amecheza michezo 116, ikishinda michezo 106, sare 31 na kupoteza michezo 29 ambapo amefunga magoli 347 na kufungwa 152 kwenye michuano yote ambayo Ufaransa imeshiriki.
#NTTupdates