×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

DKT.BITEKO KUWA MGENI RASMI MKUTANO WA 13 WA KITAALUMA WA TEF

Na Mwandishi wetu Dodoma.

NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika mkutano 13 wa kitaaluma wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), utakaofanyika kwa siku 2 kuanzia Aprili 29, 2024 jijini Dodoma.

Mkutano huo unalenga kujadili mada mahsusi na Kauli mbiu ya mkutano huo ni ‘Nafasi ya vyombo vya habari katika matumizi ya gesi kwa ajili ya kulinda misitu’, ambao utashirikisha wahariri 150 kutoka vyombo mbalimbali vya habari hapa nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari Mjumbe wa kamati ya Utendaji ya TEF, ambaye pia ni mhariri wa gazeti la FAMA Neville Meena amesema kuwa mkutano huo utafanyika jijini Dodoma kwa muda wa siku mbili.

Mjumbe huyo amesema kauli mbiu hiyo inayoongoza katika mkutano huo itatumika kama mada kuu na kwamba kutakuwa na watoa mada mbalimbali za kitaaluma ikiwamo ya wanawake na uongozi katika vyumba vya habari, nafasi zao wajibu wao pamoja na uzingatiaji wa taaluma.

“Tupo Dodoma tunajambo letu la kitaaluma ambalo litafanyika kesho jumatatu (leo), na kesho tutakuwa na mkutano kitaaluma wa 13, namada nyingine itakuwa ni kuhusu uchaguzi kama tunavyofahamu mwaka huu tutakuwa na uchaguzi wa serikali za mitaa na mwakani tukijaaliwa tutakuwa na uchaguzi wa Rais, wabunge na madiwani” amesema Meena.

Amesema watakuwa na mada hiyo kwa kuwa wanahusika na kuandika habari ikiwa ni pamoja na kuelekeza akili zao katika suala la uchaguzi huku akisema mada nyingine ni jinsi gani ya ufanyaji kazi kwa kuzingatia teknolojia inavyokua katika vyombo vya habari na watakavyokabiliana na Teknolojia ya akili Mnemba.

“Vyombo vyetu vya habari haviwezi kufanya kazi pasipo kuzingatia mabadiliko makubwa ya teknolojia,ule utawala wa magazeti, wa runinga kufikiria kila kitu kwamba bila wao kutanzangaza hakuna kitakachotokea, vyote hivyo vitaendelea kuwepo lakini tuzingatie teknolojia imekua kuna mitandao ya kijamii inafanya kazi,” amesema.

Naye mjumbe wa kamati hiyo Salim said Salim amesema kuwa waandishi wengi wanafanya habari za kiongozi fulani kapanda miti huku akisema wanandishi hao hawafuatilii maendeleo ya miti hiyo.

#NttUpdates