Na Mwandishi wetu.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Philip Mpango, amewasili Mkoani Arusha kwaajili ya kushiriki na kufungua Kongamano la Kimataifa la Watunga Sera wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii Barani Afrika litakalofanyika leo Julai 10, 2025.
Akiwasili Jijini Arusha Dkt. Mpango amepokelewa na Mkuu wa Mkoa huo Kenan Kihongosi pamoja na viongozi wengine wa Serikali ya mkoa huo.
Kongamano hilo linatarajiwa kuwashirikisha wadau wa hifadhi ya jamii kutoka nchi mbalimbali za Afrika, likilenga kubadilishana uzoefu, sera bora na mikakati endelevu ya kukuza ustawi wa jamii kupitia mifumo ya kijamii ya ulinzi.
#NTTupdates.