×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

DKT.TULIA AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA SPIKA WA FALME ZA KIARABU

Na Mwandishi wetu.

SPIKA wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), Mhe. Dkt. Tulia Ackson, leo tarehe 17 Septemba 2024, amekutana na kufanya mazungumzo na Spika wa Bunge la Umoja wa Falme za Kiarabu, Mhe. Saqr Ghobash, katika Makao Makuu ya Bunge hilo yalipo Abu Dhabi.

Katika mazungumzo yao, Viongozi hao wamejadiliana kwa kina kuhusu namna bora ya kuimarisha na kuendeleza ushirikiano mzuri uliopo kati ya Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) na nchi ya Umoja wa Falme za Kiarabu pamoja na kuangazia mahusiano kati ya Tanzania na Umoja wa Falme za Kiarabu.

Mazungumzo hayo yalijikita kwenye masuala ya ushirikiano wa kiuchumi kwa manufaa ya pande zote mbili huku lengo likiwa ni kukuza mahusiano yaliyopo ya kihistoria na kidiplomasia kwa ustawi wa wananchi wa pande zote mbili.

#NTTupdates