×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

EL NESYRI KUTIMKIA UTURUKI

Na Mwandishi wetu.

Mshambuliaji wa kimataifa wa Morocco na klabu ya Sevilla Youssef El Nesyri (27) amejiunga rasmi na miamba ya Uturuki Fenerbahce, ambapo amesaini mkataba utakao muweka klabuni hapo mpaka mwaka 2029.

El Nesyri ambaye alikuwa akiwindwa na vilabu kadhaa, huku Kocha wa Fenerbahce Jose Mourinho alihitaji mshambuliaji mwenye sifa kama za El Nesyri.

El Nesyri alijiunga na Sevilla mwaka 2020 ambapo ameichezea michezo 143 akifunga magoli 51 kwenye klabu hiyo.

#FabrizioRoman

#NTTupdates