×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

GOMES ATUA AL AHLI TRIPOLI YA LIBYA

Na Mwandishi wetu.

Klabu ya Al-Ahli Tripoli ya Libya imemtangaza Kocha wake mpya Didier Gomes Da Rosa (55) raia wa Ufaransa ambaye atakiongoza kikosi hicho kwenye ligi kuu baada ya kuachana na timu ya Taifa ya Botswana.

Gomes ambaye ana uzoefu mkubwa akiwa amefundisha vilabu kadhaa na kuacha alama kwenye vilabu hivyo ambavyo ni Rayon Sports, Simba SC, Horoya FC, Al- Alain, Ismaily na timu ya Taifa ya Mauritania na Botswana na sasa amejiunga na miamba hiyo ya Libya akichukua nafasi ya Kocha Chokri Khatoui raia wa Tunisia ambaye alifukuzwa baada ya kuondolewa na Simba SC hatua ya kwanza kusaka makundi kombe la shirikisho Afrika (CAFCC).

#NTTupdates