×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

GOR MAHIA YACHAPIKA NYUMBANI

Na Mwandishi wetu.

Klabu ya Gor Mahia ya Kenya, imejiweka kwenye mazingira magumu ya kufuzu hatua ya makundi ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL) baada ya kukubali kichapo cha magoli 3-0 kutoka kwa mabingwa mara 12 wa kombe hilo Al Ahly ya Misri.

Magoli ya mchezo huo yalifungwa na Ramy Rabia dakika ya 13 na Percy Tau aliyefunga magoli mawili dakika ya 14 na 73 baada ya walinzi wa Gor Mahia kufanya makosa mbele ya winga huyo.

Awali kabla ya mchezo huo Gor Mahia FC iliitambia Al Ahaly kupitia mitandao yao ya kijamii kuwa wataiondoa klabu hiyo kwenye hatua hiyo ya kwanza lakini mambo yamekuwa magumu kwao na wanakibarua kigumu kuiondoa Al Ahly..

#NTTupdates