×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

HATIMAE MAN UNITED YAMTIMUA TEN HAG

Na Mwandishi wetu.

Baada ya malalamiko ya muda mrefu kwa mashabiki wa klabu ya Manchester United kuhusu uwezo wa Kocha wa kikosi hicho Mholanzi Erik Ten Hag (54) hatimae mabosi wa klabu hiyo wamefikia makubaliano ya kuachana na Kocha huyo.

Kikao cha ndani cha mabosi hao, wameamua kuvunja mkataba na Kocha huyo, baada ya kutoridhishwa na matokeo ya Manchester United ukiwa ndio msimu wenye matokeo mabaya zaidi kwa mashetani hao wekundu kwenye EPL.

Ten Hag alijiunga na Man United mwaka 2022 akitokea Ajax ya nchini kwao Uholanzi na kuiongoza klabu hiyo kushinda kombe la FA na kombe la EFL msimu uliopita.

Lakini msimu huu mambo yamezidi kuwa mabaya kwa Kocha huyo baada ya kuiongoza Manchester United kwenye michezo 9 akishinda michezo 3, Suluhu 2 na kupoteza michezo 4 huku akivuna alama 11 na kushika nafasi 14 kwenye msimamo wa EPL.

#NTTupdates