Na Mwandishi wetu.
Zimesalia saa chache kushuhudia mchezo mkali wa Fainali ya mkondo wa pili wa kombe la shirikisho Afrika (CAFCC), kati ya Mnyama Simba SC dhidi ya RS Berkane ya Morocco kwenye dimba la New Amaan Complex Visiwani Zanzibar.
Simba imejipanga vyema kupata ushindi kwenye mchezo huo ili waweze kuweka historia ya kuwa timu ya kwanza kutoka ukanda wa Afrika Mashariki na kati kubeba taji hilo na kuleta heshima kwenye Taifa la Tanzania.
#NTTupdates