Na Mwandishi wetu.
Kuelekea mchezo wa Fainali ya mkondo wa pili wa kombe la shirikisho Afrika (CAFCC) kati ya Mnyama Simba SC dhidi ya RS Berkane ya Morocco, Kocha wa Mabingwa hao wa ligi kuu ya Morocco (Botola Pro), Moine Chaaban ameweka wazi kuwa hawapo tayari kupoteza mchezo huo mbele ya Simba SC.
“Tunafurahi kucheza mchezo huu dhidi ya Simba SC na mchezo wa kesho hautakuwa rahisi kwa timu zote mbili.”
“Mwaka jana tulipoteza kombe dhidi ya Zamalek, mchezo ambao umetupa uzoefu mkubwa na hatutakuwa tayari kupoteza fainali ya pili mfululizo”
Mchezo huo utapigwa hapo kesho kwenye uwanja wa New Amaan Complex Visiwani Zanzibar ambapo Simba SC ya Tanzania itawakaribisha RS Berkane ya Morocco majira ya saa 10:00, Mchezo ambao Simba SC analazimika kushinda magoli matatu bila kuruhusu wapinzani wao kupata goli ili waweze kubeba kombe hilo kwa mara ya kwanza.
#CAFCC
#NTTUPDATES