Na Mwandishi wetu.
Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za kulevya DCEA imesema, katika oparesheni zilizofanyika mwishoni mwa mwaka 2024 kwenye mwambao wa bahari ya Hindi jumla ya raia nane wa nchi ya Pakistan walikamatwa wakiwa kilogram 448.3 za dawa za kulevya wakiwa wamezificha ndani ya jahazi lililosajiliwa nchini Pakistan kwa namba BFB 16548.
Akitoa ripoti ya tathimini ya oparesheni kwa mwaka 2024, Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) Aretas Lyimo amesema Jahazi hilo lenye uwezo wa kupakia hadi tani 8 lilikuwa likisafirisha dawa za kulevya kutoka Bara la Asia na kuzileta Afrika.
#NTTUpdates