Mchezaji wa zamani wa timu ya Taifa ya uingereza na klabu ya Liverpool Jamie Carragher, ambae kwa sasa mchambuzi wa soka ameshangazwa na uamuzi wa shirikisho la soka barani Afrika (CAF) kwa kumtangaza mwenyeji wa michuano ya mataifa bingwa ya Afrika (AFCON 2025), Timu ya taifa ya Morocco kuwa bingwa wa michuano hiyo licha ya kufungwa goli 1-0 dhidi ya timu ya Taifa ya Senegal kwenye mchezo wa fainali.

“Yaani Senegal wabebe ubingwa, umati ushangilie kwa shangwe na wachezaji wanyanyue kombe, halafu uje useme, Hapana Morocco ndio mabingwa kwa mabao 3-0? Inachekesha”
Ndio maana nilisema AFCON ni mashindano madogo, Ulaya haiwezi kutokea kamwe”
Jamie Carragher akitoa maoni yake baada ya hapo jana baada ya shirikisho la soka Afrika (CAF) kuwapokonya ubingwa timu ya Taifa ya Senegal na kuwapa ushindi wa mezani Morocco kwa ushindi wa magoli 3-0.