×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

JAYRUTTY MZABUNI MPYA WA JEZI NA VIFAA VYA MNYAMA

Na Mwandishi wetu.

Klabu ya Simba SC kupitia kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Tenda ya klabu hiyo Dkt. Seif Muba ametangaza rasmi kampuni ya JAYRUTTY kuwa ndiye mzabuni wao mpya baada ya kutia Saini ya mkataba wa Bilioni 38 utakaodumu kwa miaka 5 ambapo kampuni hiyo itahusika na utengenezaji na usambazaji wa jezi pamoja na vifaa vya vyote vyenye nembo ya klabu hiyo kuanzia msimu ujao.

“Mshindi aliyeshinda tenda hiyo ameshinda kwa kuweka kiasi cha fedha cha Tsh. 38 Bilioni. Napenda kuitangaza kampuni ya Jayrutty Investment Company Limited kama mshindi.

Klabu ya Simba inakwenda kupata Tsh. 5.6 Bilioni kwa mwaka.”- Kila mwaka Simba SC itapata gawiwo la bilioni 5.6 na ongezeko la asilimia 10 kwa kila mwaka.

Aidha faida nyingine za mkataba huo ni pamoja na Ujenzi wa Uwanja wa Bunju (Watu Elf10 hadi 12), Gari la IRIZAR, Media production, Ujenzi wa Ofisi Mpya, Kukuza Vipaji ( pesa cash kutolewa), Pre seasons sponsorship (maandalizi ya msimu mpya), Medical room, Simba Day (pesa itatolewa cash milioni 100), Motisha kwa wachezaji ( M470 cash) na Jezi za brand kubwa duniani.

Maneno hayo yamesemwa na Dkt. Seif Muba Mwenyekiti wa kamati ya tenda ya Simba SC wakati akizungumza na Waandishi wa habari leo Aprili 16, 2025 kwenye hafla ya utiaji saini wa klabu hiyo na kampuni hiyo.

#NTTupdates