×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

JESHI LA POLISI ARUSHA LAJA NA ELIMU KUANZIA NGAZI YA CHINI

Na Mwandishi wetu.

Jeshi la Polisi mkoani Arusha Oktoba 21, 2024 limezindua kampeni ya “TUWAAMBIE KABLA HAWAJAHARIBIWA” kwa lengo la kutoa elimu kuanzia ngazi ya awali hadi vyuo vikuu kwaajili ya kuwaelimisha wanafunzi juu ya kujiepusha na vitendo vya uporomokaji wa maadili.

Uzinduzi huo umehudhuriwa na zaidi ya washiriki 3,000 pamoja na viongozi mbalimbali akiwemo Katibu Tawala Msaidizi viwanda, Barabara na Uwekezaji Mkoa wa Arusha Bw. Frank Mbando ambaye amemuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Arusha Paul Christian Makonda.

Bw. Frank Mbando amewataka wanafunzi kujua na kufahamu vyema kuwa wao ndiyo Taifa la kesho hivyo wanakila sababu ya kutambua rika waliopo hivi sasa wanapaswa kuwa makini ili kuepukana na vitendo hatarishi kwa maisha yao ya sasa na baadae.

Aidha amebainisha kuwa Serikali inayoongozwa na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan itaendelea kutoa elimu kwanzia ngazi ya chini zaidi ili kuhakikisha wanafunzi wote wanapata elimu yenye ubora bure ambapo amesema hadi kufikia sasa kiasi cha Shillingi Billion saba zimeshatolewa kwaajili ya elimu tangu Serikali ya awamu ya sita imeingia madarakani.

Nae, Mkuu wa wa Dawati la Jinsia na Watoto Mkoa wa Arusha Mrakibu wa Polisi SP Happiness Temu ameweka wazi juu ya lengo la kampeni hiyo kuwa ni kuwatahadharisha wanafunzi wa shule za awali, msingi, sekondari pamoja na vyuo vikuu kuacha kuiga tabia ambazo hazina manufaa na tija kwao binafsi pamoja na Taifa.

#NTTupdates