Na Mwandishi wetu.
Jeshi la Polisi mkoani Arusha limetoa taarifa ya awali juu ya taarifa inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii ikimuonyesha mwanamke mmoja aitwae Mercy Daniel, mkazi wa Arusha akielezea kupotelewa na mume wake aitwae David Gipson ambaye pia ni mkazi wa Arusha na kuweka wazi kuwa Jeshi hilo halijamshikilia mtu huyo.
Akitoa taarifa hiyo leo Machi 18, 2025 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Justine Masejo amesema kuwa Jeshi hilo limeipokea taarifa hiyo na tayari uchunguzi wa shauri hilo unaendelea huku akibainisha kuwa uchunguzi wa awali umebaini kuwa David Gipson amehusishwa na upotevu wa fedha uliotokea siku za karibuni katika moja ya benki mkoani humo ambapo jina la benki hiyo limehifadhiwa kwaajili ya uchunguzi wa kina zaidi.
Aidha, SACP Masejo amewataka wananchi kutoa ushirikiano kwa Jeshi hilo wakati wowote watakapomuana mtu huyo lakini pia kuendelea kutoa taarifa za uhalifu ndani ya mkoa huo.
#NTTupdates.