×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YATUA NGORONGORO

Na Mwandishi wetu.

Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii leo Machi 13, 2025 wakiongozwa na Mwenyekiti wao, Timotheo Mnzava pamoja na Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi, Dkt. Pindi Chana wamefika eneo la ujenzi wa ofisi mpya ya Hifadhi ya Ngorongoro na kukagua mwenendo wa ujenzi huo.

Ofisi hiyo mpya inajengwa nje ya hifadhi ya Ngorongoro inagharimu takribani shillingi Billion 10.5 za Kitanzania ambapo hadi sasa utekelezaji wake umefikia 85% huku ikitarajiwa kukamilika ifikapo Mei 30, 2025.

Kamati hiyo ipo Jijini Arusha kwaajili ya ukaguzi wa miradi mbalimbali iliyopo chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii.

#NTTupdates.