×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

KANE MCHONGO WA MAKOMBE BADO HAUJATIKI

Na Mwandishi wetu.

Mshambuliaji wa timu ya Taifa ya Uingereza na klabu ya Bayern Munich ya Ujerumani Harry Kane (31), ameendelea kupishana na makombe barani Ulaya baada ya timu yake kushindwa kufuzu nusu fainali ya ligi ya Mabingwa Ulaya (UEFA), baada ya kuondolewa na Inter Milan ya Italia kwa jumla ya magoli 4-3.

Harry Kane ambaye alijiunga na Bayern Munich mwanzoni mwa msimu huu akitokea Tottenham Hotspur amefunga magoli 11 na kutoa assist 2 kwenye michezo 13 ambayo ameichezea Bayern Munich katika michuano ya ligi ya Mabingwa Ulaya UEFA msimu huu.

Kane hajawahi kubeba kombe lolote la ubingwa wa ligi kuu wala ligi ya Mabingwa Ulaya (UEFA), alijiunga na Bayern Munich akiamini atabeba makombe lakini sasa amesalia na kombe moja pekee la ligi kuu ya Ujerumani (Bundesliga).

#NTTUPDATES