×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

KAULI YA CHALAMILA YAMUIBUA MBUNGE ” RC ANASEMA MUITE MUMEO AJE AKUSAIDIE KUJIFUNGUA?

Na Mwandishi wetu.

Mbunge wa viti Maalum Annatropia Teonist leo Januari 31, 2025 bungeni jijini Dodoma ameitaka Serikali itoe kauli kuhusu wanawake ambao wanakosa vifaa vya kujifungulia.

Amesema kukosa vifaa hivyo mama anaweza kupata maambukizi,lakini pia hata kupelekea umauti.

“Ni majuzi tu tumesikia kauli ya Mkuu wa Mkoa akieleza alivyomjibu mjamzito ambae hakuwa na vifaa vya kujifungulia akitoa kauli za kukatisha tamaaa kwamba aende mumewe akamsadie kujifungua ni kauli gani hizi?anahoji Annatropia

Akijibu swali hilo Naibu waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel amesema, Serikali imetoa maelekezo mahususi, huku maagizo katika hospitali hizo yakiwa ni kipaumbele cha kwanza kabisa ni huduma kwanza gharama badae.

#NTTupdates