×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

KIMYAA KAMA HAUPO NUSU FAINALI (UEFA)

Na Mwandishi wetu.

Klabu ya Arsenal imeendeleza ubabe wake kwa Mabingwa wa kihistoria wa ligi ya Mabingwa Ulaya (UEFA), Real Madrid baada ya kupata ushindi wa magoli 2-1 kwenye mchezo wa marudiano hatua ya Robo fainali uliopigwa kwenye dimba la Santiago Bernabeu, jijini Madrid, nchini Hispania.

Ushindi huo umewafanya Arsenal kutinga hatua ya nusu fainali kwa jumla ya ushindi wa magoli 5-1 ambapo watakutana na Mabingwa wa ligi kuu Ufaransa (League 1) Paris-Saint+German ambayo imefika hatua hiyo baada ya kuziondoa timu mbili za EPL ambazo ni Liverpool na Aston Villa.

Pia mchezo huo ulishuhudia nyota wa Real Madrid Mbappe akitolewa dakika ya 74′ na nafasi yake ulichukuliwa na Brahim Diaz baada ya kupata majeraha.

#NTTupdates