Na Mwandishi wetu.
Dakika 90 zimemalizika kwenye uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mkoani Tabora na kushuhudia Mnyama Simba SC akitakata ugenini baada ya kupata ushindi mnono wa magoli 3 -0 kwenye mchezo huo.
Magoli ya Simba SC yamefungwa na mshambuliaji Lionel Ateba ambaye alifunga magoli mawili dakika ya 12 na dakika ya 34 kwa mkwaju wa penati huku goli la tatu likifungwa na mlinzi wa kulia Shomari Kapombe dakika ya 66.
Simba SC wamerejea kileleni mwa msimamo wa ligi kuu NBC baada ya kufikisha alama 43 wakiwashusha watani wao wa jadi Young Africans SC wenye alama 42.
#NTTupdates