
Na Mwandishi wetu.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Paul Christian Makonda amemuapisha Lameck Ng’ang’a kuwa Mkuu mpya wa Wilaya ya Karatu akichukua nafasi ya Dadi Kolimba ambaye alihamishiwa kwenda Wilaya ya Tanga.
Uapisho huo umefanyika hii leo Mei 21, 2025 katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo ambapo kabla ya kuteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya hiyo Lameck Ng’ang’a alikuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Karatu.



#NTTupdates.