Na Mwandishi wetu.
Beki wa kushoto wa timu ya Taifa ya Tunisia na nahodha wa klabu ya Al Ahly ya Misri, Ali Maaloul (34) anatarajiwa kuondoka klabuni hapo mwishoni mwa msimu huu mkataba wake utakapomalizika na kurejea nyumbani kwao Tunisia.
Maaloul ambaye alijiunga na Al Ahly mwaka 2016 akitokea CS Sfaxien ya Tunisia baada ya kuwa na msimu Bora Tunisia akibeba tuzo ya mfungaji Bora licha ya kuwa mlinzi wa kushoto kwenye klabu yake.
Maaloul akiwa Al Ahly amebeba makomba 21 ambapo Makombe 6 ya ligi kuu Misri, Makombe 4 ya ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL), Makombe 4 Egypt Cup, Makombe 2 ya CAF Super Cup, na Makombe 5 ya Egypt Super Cup.
Nyota huyo anatarajiwa kujiunga na timu yake ya zamani ya CS Sfaxien kumalizia safari yake ya soka ambayo imempatia mafanikio makubwa na miongoni mwa wachezaji wanaopewa heshima kubwa nchini Tunisia.
#NTTupdates