Na Mwandishi wetu.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa, ametangaza rasmi kutogombea tena ubunge katika Jimbo la Ruangwa, mkoa wa Lindi, baada ya kulitumikia kwa muda wa miaka 15.
Uamuzi huo umeibua hisia mbalimbali miongoni mwa wananchi na wafuasi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), wakimtambua kama kiongozi aliyetoa mchango mkubwa katika maendeleo ya jimbo hilo na taifa kwa ujumla.
Taarifa ya kutogombea ubunge imetolewa na Katibu wa CCM Wilaya ya Ruangwa, Abbas Makwetta, aliyebainisha kuwa Majaliwa amefikia uamuzi huo kwa hiari yake mwenyewe.
Alisema kuwa kiongozi huyo ameonesha mfano wa kuigwa kwa kuhitimisha kipindi chake kwa heshima na kuacha nafasi kwa viongozi wapya kuchangia maendeleo ya eneo hilo.
Katika kipindi cha uongozi wake, Majaliwa amesimamia miradi mingi ya maendeleo ikiwemo sekta za elimu, afya, miundombinu na maji. Wengi wanamkumbuka kama kiongozi mchapakazi, mwenye nidhamu ya hali ya juu na maono ya kimkakati katika kukuza ustawi wa wananchi wa Ruangwa.
Uamuzi wake wa kuachia ngazi unaacha alama ya heshima na mafanikio ambayo yataenziwa kwa muda mrefu.
#NTTupdates