×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

MAMA WA MAPACHA 4 ARUSHA, AOMBA SERIKALI NA WADAU KUMSAIDIA MAHITAJI YA WATOTO

Arusha Mama wa mapacha 4 Janeth Manota 27 ameomba serikali pamoja na wadau mbalimbali kumsaidia mahitaji ya kuwalea watoto wake aliojifungua hivi karibuni katika hospitali ya rufaa ya Mt.meru kwa njia ya upasuaji kwa kuwa hana uwezo wa kuwahudumia kimahitaji Mwanamke huyo mkazi wa Morombo jijini Arusha alijifungua Novemba 26,2023 ikiwa ni uzao wake wa pili na watoto wote wana afya njema na uzito mzuri wa kilogram 1.4, 1.5, 1.8 na 1.9.

Janeth anasema mimba ya mapacha hao wa nne ilikuwa na changamoto kubwa ya yeye kuishiwa na damu,kuumwa mgongo na kichwa na alipumzishwa kitandani tangu mimba ikiwa na miezi minne hadi kujifungua.

“Hofu yangu kubwa kwa sasa ni namna ya kuwalea wanangu kwa mahitaji mbalimbali naomba serikali na wadau wajitokeze kunisaidia ili niweze kuwalea vizuri”anasema Janeth Mkuu wa Wilaya ya Arusha ,Felician Mtahengerwa alisema serikali ya wilaya imeanza kuchukua hatua ya kumsaidia namna ya kulea watoto hao ikiwemo kuwakatia Bima ya Afya na wadau mbalimbali wameonesha nia ya kusaidia malezi ya wapacha hao.

#NTTUpdates