×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

MAN UNITED KUMUWEKA SOKONI ANTONY

Na Mwandishi wetu.

Mashetani wekundu, Manchester United imepanga kumtoa kwa mkopo winga wao wa kulia Antony Mathieus dos Santos (24) raia wa Brazil kwenye dirisha lijalo la usajili au kumuuza jumla.

Man United imepanga kumuuza winga huyo kwa dau la paundi Milioni 40 kwa klabu yoyote itakayokuwa inamuhitaji mchezaji huyo ambaye amekuwa hana nafasi ya kudumu kwenye kikosi cha kwanza kwa Kocha Erik Ten Hag ambaye ndiye alipendekeza usajili wa winga huyo.

Antony alijiunga na Manchester United mwaka 2022 akitokea klabu ya Ajax, Uholanzi ambapo united ilimnunua kwa paundi Milioni 85.

#NTTupdates