×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

MANUEL NEUER AVUNJIKA MBAVU

Na Mwandishi wetu.

Habari mbaya kwa Mashabiki wa Bayern Munich nchini Ujerumani baada ya taarifa ya kuwa mlinda lango namba moja wa klabu hiyo Manuel Peter Neuerb(38) raia wa Ujerumani amepata majeraha ya mbavu na atakosekana mpaka Januari mwakani.

“Manuel Neuer atakosa mechi zijazo za Bayern Munich amevunjika mbavu, Pengine hatacheza tena mwaka huu. Jambo kuu ni sasa kupona. Kisha tunatumai kuwa tutamrejesha Manuel Januari,”

Maneno yamesemwa na Kocha wa kikosi hicho raia wa Ubelgiji Vincent Kompany kwenye mkutano na Waandishi wa habari.

Kabla ya majeraha Manuel Neuer msimu huu ameichezea Bayern Munich michezo 19, akiruhusu magoli 13 akitoka na Cleensheet 12 huku akipewa Kadi nyekundu moja kwenye mchezo wa DFB Pokal dhidi ya Leverkusen.

#NTTupdates