Na Mwandishi wetu.
Mke wa Rais wa Zanzibar, Msarifu na Mwenyekiti wa Bodi ya wadhamini ya Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation (ZMBF) Mama Mariam Mwinyi amesema wakati umefika kwa Wadau kuunganisha nguvu za pamoja kuwasaidia Wanafunzi wa Kike Kutimiza ndoto zao za Kielimu.
Ametoa rai kwa wadau zaidi kuunga Mkono Juhudi za Kumaliza Changamoto wanazokabiliana nazo watoto wa Kike wanapokuwa Skuli.
Mama Mariam Mwinyi ameyasema hayo katika ufunguzi wa Skuli Mpya ya Msingi Kojani ,Wilaya Ndogo Kojani, Mkoa wa Kaskazini Pemba.
Mama Mariam ameeleza kuwa Taasisi ya ZMBF tangu Mwaka 2022 imekuwa na Utaratibu wa Kugawa Taulo za kike kwa Wanafunzi wa Kike na tayari imewafikia Wanafunzi 5,676 Unguja na Pemba.
Aidha amesisitiza kuwa Taasisi hiyo Imeandaa Programu Mpya yenye lengo la kuwapatia Wanafunzi wa kike 3000 taulo za kike na tayari imewafikia Wanafunzi 643 wa Wilaya ya Kusini na Kati Unguja.
Amefahamisha kuwa Wanafunzi wengi wa kike wamekuwa wakikabiliana na Changomoto nyingi zinazodhorotesha kiwango chao cha Elimu ,Utorò na Kukatisha Masomo hususani wanapokuwa katika Ada zao Za Mwezi.
Halikadhalika Mama Mariam Mwinyi amesema taasisi hiyo imepanga Tumaini Kit 777 , Soksi na Viatu jozi 5,548 watapatiwa Wanafunzi wa kike wa Skuli za Msingi na Sekondari za Kojani.
Hafla hiyo ya Ufunguzi wa Skuli ya Kojani iliambatana na Ugawaji wa taulo za Kike kwa Wanafunzi wa Kike wa Kojani.
Ufunguzi huo wa Skuli ya Msingi Kojani ni Miongoni mwa Shamrashamra za Sherehe za Miaka 61 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
#NTTUpdates