
Mabingwa watetezi wa ligi kuu ya NBC Young Africans SC, imewaomba mashabiki zake kudumisha ustaarabu wanapokwenda viwanjani kushangillia timu yao inapocheza.
“Nimeona ni vyema leo kuzungumza na Wanachama pamoja na Mashabiki wetu. Jana jioni, kupitia taarifa ya Bodi ya Ligi, sote tulishuhudia adhabu ya faini iliyotolewa kufuatia vitendo vya baadhi ya Wanachama na Mashabiki wetu kurusha chupa uwanjani katika michezo wetu wa ugenini dhidi ya Azam FC”.
“Hii ni mara ya pili kwa Klabu yetu kutozwa faini ya aina hii. Ni muhimu kufahamu kuwa adhabu hizi zina athari kubwa kifedha na zikiendelea mwisho wake hautakuwa mzuri kwa maendeleo ya Klabu yetu.
Napenda kuwaomba Wanachama na Mashabiki wetu wote kudumisha ustaarabu wanapofika uwanjani kuishangilia Klabu yetu. Furaha inapopatikana, tushangilie na pale ambapo kuna jambo halijaridhisha, tunaweza kuonesha hisia zetu kwa njia za amani kama vile kusoma lakini si kwa kurusha chupa au vitu vingine hatarishi wala kusababisha fujo.
Vitendo vya namna hiyo havina nafasi katika soka letu na si sehemu ya utamaduni tunaotaka kuujenga.
Tushirikiane kulinda taswira ya Klabu yetu na kuhakikisha mazingira ya uwanjani yanabaki kuwa salama yenye heshima na yanayovutia kwa kila mmoja.
Ally Kamwe, meneja habari na mawasiliano wa klabu ya Young Africans SC akizungumza na waandishi wa habari kuelekea mchezo wao wa kesho dhidi ya Mtibwa sugar.
@YangaSC