Na Mwandishi wetu.
Klabu ya Tottenham Hotspur ya Uingereza imefanikiwa kumpata kwa mkopo winga wa kushoto Mathys Henri Tel (19) raia wa Ufaransa akitokea Bayern Munich ya Ujerumani.
Tel ambaye hajawa na wakati mzuri kwenye kikosi Cha Bayern Munich chini ya kocha Vicent Kompany amejiunga na Spurs ili kupata nafasi zaidi ya kucheza na kuendeleza kipaji chake Uingereza.
Tel amecheza michezo 14 akitoa assist moja pekee kwenye michuano yote ambayo klabu ya Bayern Munich imeshiriki msimu huu.
#NTTupdates